Hatimaye msanii wa Bongofleva, Rayvanny ameiaga rasmi lebo ya WCB Wasafi ambayo alikuwa akifanya nayo kazi zake za kimuziki
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amemshukuru boss wa lebo hiyo msanii Diamond Platnumz kwa nafasi aliyompa.
“Thank You wcb_wasafi ” – Ameandika Rayvanny ambaye hupenda kujiita Chui.
Ikumbukwe, Rayvanny alisainiwa na WCB mwaka 2016, na tangu awe chini ya lebo hiyo ameachia ngoma nyingi, ikiwemo album moja pia ameacha alama ya mafanikio makubwa kama kushinda tuzo ya BET mwaka 2017, kutumbuiza kwenye tuzo za MTV EMA