Mwanamuziki Rayvanny ameongeza tuzo katika kabati lake la tuzo baada ya kushinda tuzo ya Hipipo Music Award katika kipengele cha African Best Act 2021.
Tuzo hizo kutoka Uganda zimemtaja Rayvanny kushinda tuzo kupitia wimbo wa Mama Tetema ambao ameshirikishwa na mwanamuziki kutoka Colombia Maluma, wimbo ambao ni Remix version ya wimbo wake wa Tetema.
Wimbo huo uliachiwa rasmi Novemba 12 mwaka huu ambapo ulitambulishwa kwenye Jukwaa la Tuzo za MTV EMA na kumfanya Rayvanny kuwa msanii wa kwanza Barani Afrika kufikia hatua hiyo.