You are currently viewing Rayvanny ashinda tuzo ya Diafa, Dubai

Rayvanny ashinda tuzo ya Diafa, Dubai

Mwimbaji wa Bongofleva toka Next Level Music (NLM), Rayvanny ameshinda tuzo za Diafa kutokea Dubai usiku wa kuamkia leo.

Rayvanny anakuwa msanii wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kupokea Tuzo hiyo ambayo hutolewa kuwaheshimisha watu mashuhuri mbali mbali toka falme za Kiarabu na hata Kimataifa kufuatia mafanikio na mchango wao kwa mwaka mzima katika Kusaidia na kuboresha Jamii. Tuzo za kwanza zilifanyika 2017.

Kwenye Tuzo za mwaka huu ambazo zilitolewa Novemba 4, zilijumuisha ‘honorees’ kutoka mataifa 18 ikiwemo Ufaransa, Tanzania, Pakistan, India, Tunisia, Saudi Arabia na mengine.

Washindi huchaguliwa na kamati maalum yenye uweledi kwenye nyanja tofauti kama Muziki, Sanaa, Utamaduni, Biashara, Kazi za Kijamii na kadhalika.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke