You are currently viewing Rayvanny atajwa kuwania tuzo kubwa za Kilatini

Rayvanny atajwa kuwania tuzo kubwa za Kilatini

Boss wa lebo ya ‘Next Level Music’, msanii Rayvanny kufuatia ametajwa kwenye tuzo kubwa za Kilatini ziitwazo “Lo Nuestro Awards”.

Waandaaji wa tuzo hizo kupitia kurasa zao za mitandao ya Kijamii Premiolonuestro wametangaza majina ya wasanii waliochaguliwa kuwania mwaka huu kupitia vipengele mbalimbali. Majina ya wanamuziki wakubwa Dunianii yamehusu sana akiwemo pia Mtanzania pekee Rayvanny akiiwakilisha vyema Afrika Mashariki kwa ujumla.

Rayvanny amechaguliwa kuwania kwenye Kipengele cha Wimbo Bora wa Mwaka “Song of the Year (Urbun pop)” kupitia wimbo wake “Mother tremble” ambao ni Mama Tetema akiwa na Maluma.

Tuzo hizo za 35 mwaka huu, zinatarajiwa kutolewa Februari 24 ndani ya Miami-Dade Arena, huko Miami, Florida nchini Marekani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke