Mwanamuziki na C.E.O wa record label ya Next Level Music Rayvanny ametajwa na mtandao maarufu wa Forbes Africa katika orodha ya wanamuziki 20 kutoka barani Africa wanaotabiriwa kufanya vizuri katika muziki wa Afrika (future of the african music).
Rayvanny ametajwa kwenye orodha hiyo sambamba na wasanii wengine wakubwa afrika kama Diamond Platnumz Burnaboy, Davido, Wizkid, Angelina Kidjo, Black Cofee, Tiwa Savage na wengine.
Orodha hii ya Forbes imetaja kuzingatia uwakilishi na uhusika wa wasanii husika katika matamasha na tuzo kubwa za muziki kama Grammy.