Mshindi pekee wa tuzo ya BET Tanzania na Mkurugenzi wa lebo ya Next Level Music Rayvanny ameachia EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Flowers 2.
Rayvanny ameamua kuwa surprise mashabiki zake kwa kuachia EP hiyo mpya yenye nyimbo tisa huku akiwa amewashirikisha wasanii mbalimbali kama marioo, nadia mukami, zuchu, ray c, guchi na Roki.
EP hiyo ni muendelezo wa EP yake ya kwanza ya Flowers iliyotoka mwanzoni mwa mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya nyimbo 8.
Lakini pia ni EP ya tatu kwa mtu mzima Rayvanny baada ya new chui ep aliyotoka,mwaka wa jana ikiwa na jumla mikwaju sita ya moto.
Mpaka sasa Rayvanny ana jumla ya EP tatu na Album moja ambayo ni Sound from Africa iliyotoka mwaka huu 2021