You are currently viewing Rayvanny awashukuru mashabiki kwa kushinda tuzo ya Zikomo nchini Zambia

Rayvanny awashukuru mashabiki kwa kushinda tuzo ya Zikomo nchini Zambia

Msanii wa Bongofleva Rayvanny amewashukuru mashabiki wake baada ya album yake “Sound from Africa” kushinda tuzo za Zikomo nchini Zambia kama Album Bora ya Mwaka.

Boss huyo wa lebo ya NLM Rayvanny aliachia rasmi album yake “Sound from Africa” Februari Mosi, 2021 ikiwa ndio album yake ya kwanza katika safari yake ya muziki. Ina jumla ya nyimbo 23 alizowashirikisha wasanii 20 kutoka Tanzania na nchi nyingine za Afrika.

Itakumbukwa, Album ya “Sound from Africa” iliweka rekodi Afrika Mashariki kwa kufikisha wasikilizaji zaidi ya Milioni 100 ndani ya wiki moja pekee tangu itoke. Ikijumuisha wasikilizaji kutoka mitandao ya Audiomack, Boomplay, iTunes, Spotify, YouTube, Boomplay na Apple Music.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke