You are currently viewing RAYVANY ATANGAZA UJIO WA TOUR YA MSANII WAKE MACVOICE

RAYVANY ATANGAZA UJIO WA TOUR YA MSANII WAKE MACVOICE

Msanii wa bongofleva Rayvanny ameweka wazi ujio wa tour ya kimuziki ya msanii wake MacVoice ambaye ana mwezi mmoja tangu atambulishwe rasmi kuwa chini ya lebo ya Next Level Music.

Rayvanny ambaye ni boss wa Next Level Music amebainisha ujio huo kupitia Insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kwa kuandika  ujumbe unaosomeka “Macvoice tour.. Show time” akiambatanisha na emoji za moto.

MacVoice ambaye ni nyota mpya wa kizazi kipya nchini Tanzania, tayari ana EPmoja ambayo ni ‘Voice’ yenye jumla ya mikwaju 6  ya moto ikiwemo bonus track moja.

Kubwa zaidi MacVoice anawania tuzo ya All Africa Music Awards kupitia kipengele cha Msanii Bora Chipukizi wa mwaka 2021 ambapo anachuana na wasanii wengine kutoka nchi za Afrika wakiwemo Omah Lay, Liya, Guchi, Oxlade na wengine wengi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke