You are currently viewing RECHO RAY AKIRI USHIRIKINA KUSHEHENI KWENYE MUZIKI WA UGANDA

RECHO RAY AKIRI USHIRIKINA KUSHEHENI KWENYE MUZIKI WA UGANDA

Msanii Recho Ray amefunguka na kudai kwamba tasnia ya muziki nchini Uganda imesheheni ushirikina.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Recho amesema nguvu za giza ndio chanzo ya baadhi ya wasanii wakongwe nchini humo kusalia kwenye muziki kwa muda mrefu.

Mrembo huyo amesema wasanii wengi wenye vipaji wamepotea kimuziki kutokana na baadhi ya wadau nchini Uganda kutumia hirisi kuua mafanikio yao.

Recho Ray ambaye ulimwengu wa muziki ulimfahamu mwaka 2018 kupitia wimbo wake uitwao “Who is Who” amekuwa akisuasua kwenye muziki wake bila kuachia hitsong yeyote.

Utakumbuka mrembo huyo sio msanii wa kwanza kudai kuwa kiwanda cha muziki nchini Uganda imetawala ushirikina, miezi kadhaa iliyopita msanii Nince Henry aliibuka na kuwatolea uvivu wasanii wote wanaoishi Makindye kwa tuhuma za kuwadhamini sana waganga wa kienyeji kwenye suala la kusafisha nyota yao ya muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke