You are currently viewing RECHO REY AKANUSHA MADAI YA KUTOA UJA UZITO

RECHO REY AKANUSHA MADAI YA KUTOA UJA UZITO

Female Rapper kutoka nchini Uganda Recho Rey amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa alitoa  uja uzito wake mwaka wa 2021.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Recho Rey amesema uvumi wa yeye kuavya mimba ulianza mara baada tumbo lake kupungua jambo ambalo amelikanusha kwa kusema kuwa hajawahi toa uja uzito wowote katika maisha yake ila kipindi hicho alikuwa anapitia changamoto nyingi katika maisha.

Mrembo huyo amesema kuwa alipatwa na msongo wa mawazo kutokana na kuvulia kiuchumi hii ni baada ya uongozi wake kusitisha mkataba wa kusimamia muziki wake kipindi cha korona.

Utakumbuka kwa sasa Recho Rey yupo mbioni kutafuta uongozi mwingine ambao utasimamia kazi zake za muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke