You are currently viewing RED BANTON AKANUSHA KUKWEPA KULIPA KODI

RED BANTON AKANUSHA KUKWEPA KULIPA KODI

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka Uganda Red Banton amekanusha tuhuma zinazosambaa mtandaoni kuwa amekuwa akikwepa kulipa kodi.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Red Banton amesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote kwani ilikuwa ni njia ya wakosoaji wake kumchafulia jina.

Aidha amesema tangu taarifa hizo zilipoibuliwa mtandaoni amefaidi pakubwa na pesa nyingi kutoka kwa wasamaria wema pamoja na marafiki zake wa karibu.

Kauli ya Red Banton imekuja mara baada ya mwanamke mmoja mmiliki wa nyumba kuibuka na kumuanika Red Banton mtandaoni kwa kusema kwamba amekuwa akikwepa kulipa kodi ya nyumba anayoishi kwa muda mrefu baada ya kuingiwa na jeuri.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke