You are currently viewing Refigah awatolea uvivu wasanii wa Kenya kwa kuhujumu jitihada za kufufua tasnia ya muziki

Refigah awatolea uvivu wasanii wa Kenya kwa kuhujumu jitihada za kufufua tasnia ya muziki

Mwanzilishi wa Grandpa records Noah Yusuf, maarufu Refigah ameandika barua ya wazi kwa wasanii wa Kenya.

Kwa mujibu wa Refigah, kuzorota kwa hali ya muziki nchini kutawafanya wasanii chipukizi kukata tamaa kwenye harakati za kutoka kimuziki kutokana na mazingira magumu.

Refigah kupitia taarifa yake anasema kwa sasa muziki wa kenya haufanyi vizuri sokoni na kila jitihada zinazofanywa na wadau husika kufufua tasnia ya muziki zinahujumiwa na baadhi ya wasanii.

Aliwashutumu wasanii wa Kenya kwa kuishi maisha ya kuigiza kwenye mitandao yao ya kijamii huku akiongeza kuwa wasanii wengi wamekuwa wakitafuta njia ya kusaidiwa na serikali kama wasanii binafsi jambo ambalo anasema linaua tasnia ya muziki nchini.

Kulingana na msanii huyo wa muziki, wakati waziri wa MNichezo na Sanaa Ababu Namwamba alipowapa wasanii fursa ya mazungumzo, hakuna aliyeheshimu mwaliko huo huku baadhi wakiomba shilingi 5,000 ya mafuta ya magari yao.

Hata hivyo anadai kuwa wasanii wengi walifanya hivyo kwa kupenda na si kunufaisha tasnia ya muziki huku akimhimiza Ababu Namwamba asikate tamaa katika ajenda ya kufufua tasnia ya muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke