You are currently viewing REKLESS ASITISHA SHOW YAKE GHAFLA HUKO MUMIAS

REKLESS ASITISHA SHOW YAKE GHAFLA HUKO MUMIAS

Msanii wa kundi la Ethics Entertainment, Rekless amewaacha mashabiki zake wa Mumias na maswali mengi baada ya kujiondoa dakika ya mwisho kwenye onesho la Mumias Cultural Center.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rekless amesema uongozi wake umechukua maamuzi magumu kusitisha show hiyo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao huku akiwaomba radhi mashabiki ambao kwa njia moja au nyingine wameathirika pakubwa na uamuzi huo.

“We made this difficult decision to cancel Mumias cultural center event because of unavoidable circumstances. We understand that this change may cause great inconvenience to my fans and we are sincerely sorry.” Ameandika kwa masikitiko kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Utakumbuka hii si mara ya kwanza kwa Rekless kuwaacha mashabiki njia panda,mapema mwaka huu alisusia show yake huko Lodwar, kaunti ya Turkana baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na waandaaji wa show hiyo kwenye ishu ya malipo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke