You are currently viewing REMA NAMAKULA MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

REMA NAMAKULA MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini uganda Rema Namakula ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo amekuwa akiifanyia kazi kwa muda mrefu.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Rema amedokeza kwamba yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya kukamilisha album yake mpya ambayo itaingia sokoni mwaka huu wa 2022.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Katonotono” amesema amekuwa akitumia muda wake mwingi studio kuitayariasha album yake mpya  ambayo kwa mujibu wake amesema ni moto wa kuotea mbali, hivyo mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea album yake hiyo.

Utakumbuka tangu Rema Namakula ajifungue mtoto wake na Dr. Hamzah Sebunya amekuwa kimya kwenye masuala ya kuachia muziki kwa ajili ya kuishughulikia familia yake.

Kazi ya mwisho kutoka kwa Rema Namakula ilikuwa ni ngoma iitwayo Akafe Che ambayo ndani kipindi cha miezi mitatu imefikisha zaidi ya views millioni 1.5 kwenye mtandao wa youtube.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke