You are currently viewing REUBEN KIGAME AKOSOA SERIKALI YA RAIS WILLIAM RUTO KISA DINI

REUBEN KIGAME AKOSOA SERIKALI YA RAIS WILLIAM RUTO KISA DINI

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Reuben Kigame amedai kuwa rais William Ruto ameanza kusahau majukumu yake kwa kuendekeza sana masuala ya dini kwenye uongozi wake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter mwiimbaji huyo aliyegeukia siasa amesema sio mbaya kwa rais huyo wa Kenya kuwa mlokole, ila anapaswa kuongoza nchi kwa mujibu wa kifungu cha 27 ya katiba.

Kigame amesema licha ya kwamba yeye ni mkristo, suala la kumpunguzia mwananchi wa kawaida gharama ya maisha haiwezi suluhishwa kwa maombi pekee bali inamuhitaji rais wa nchi kutengeneza mazingira rafiki ya kumuondolea mkenya mzigo huo.

Hata hivyo tweet yake imezua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo baadhi wameonekana kumuunga mkono kwa malalamiko yake dhidi ya serikali huku wengine wakimtaka aache masuala ya siasa na badala yake arudi kwenye kazi yake ya kumtumkia Mungu kupitia uimbaji.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke