You are currently viewing RHINO KING ATAMANI KUZICHAPA NA HARMONIZE ULINGONI

RHINO KING ATAMANI KUZICHAPA NA HARMONIZE ULINGONI

Mwanamuziki wa Bongfleva Rhino King ameweka wazi kutamani kupigana na msanii mwenzake Harmonize kufuatia kauli ya Bosi huyo wa Konde Gang aliyoitoa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rhino King ameibuka na kumjibu Harmonize kwamba yupo tayari kwa pambano hilo huku akimtaka atangaze tarehe watakayoingia ulingo kuzichapa.

“Ulitangaza nakujigamba kwamba uko fiti na unataka pambano na yeyote kwenye game, niko hapa Tyson Faru, tayari kabisa kwa pambano na wewe kivyovyote. Tangaza tarehe uliemtaka umeshampata no excuses please nishakutamani” Unasomeka ujumbe wa Rhino King kupitia ukurasa wake.

Utakumbuka, Harmonize siku ya Ijumaa alishare video fupi kupitia insta story yake anayoonekana akiwa gym akifanya mazoezi makali ya ngumi huku akitaka mtu yeyote mwenye matatizo naye binafsi wakamalizane ulingoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke