Msanii aliyekuwa akiunda kundi la the Mafik, Rhino ameweka wazi juu ya hatma ya kundi hilo kufanya kazi kwa pamoja kama ilivyokua awali.
Akitumia ukurasa wake wa Instagram kujibu maswali ya mashabiki waliotaka kujua hatma ya kundi hilo lililofanya vizuri na wimbo wa passenger, rhino amejibu kua kundi hilo halipo tena wala halitakuja kuwepo tena.
Ikumbukwe kundi la the mafik lilikuwa linaundwa na wasanii Rhino, mbala mwezi na Hamadai lakini tangu msanii mbala mwezi Afariki mwaka wa 2019 kundi hilo limekuwa likisuasua kimuziki.
|