You are currently viewing RICH MAVOKO ASOGEZA MBELE TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

RICH MAVOKO ASOGEZA MBELE TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva, Rich Mavoko amehairisha tarehe ya kuachia albamu yake mpya, iitwayo Fundi ambayo ilipaswa kutoka Machi 18 mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Rich Mavoko amesema amesogeza mbele tarehe ya kuachia albamu yake mpya hadi Machi 25 mwaka huu kwa ajili ya kutoa heshimu kwa aliyekuwa rais wa awamu ya tano nchini Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli ambaye wiki hii Watanzania wamefanya makumbusho yake  ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu afariki dunia.

“Album ya Fundi ilitakiwa itoke kesho Tarehe 18 March lakini ni vyema zaidi kuchukua siku hizi kuyakumbuka yale makubwa na ya kihistoria yaliofanyika na mpendwa wetu Dkt John Pombe Magufuli.

“Aligusa maisha ya wengi na wengi bado tunamkumbuka, hatuna budi kushukuru na kuendelea kumuombea amani popote alipo! FUNDI itakufikia popote ulipo tarehe 25 March 2022.” Ameandika Rich Mavoko

Utakumbuka album ya Fundi ndio album ya kwanza kwa mtu mzima Rich Mavoko tangu aanze safari yake ya muziki licha ya kuachia mini-tape yenye jumla ya ngoma 7 za moto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke