Mtandao wa MTO News umeripoti kuwa Rapper Rick Ross yupo kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi na msanii wake ambae pia ni rapper Pretty Vee.
Mapema mwaka huu, Rozay alimsaini Pretty Vee katika record label yake ya Maybach Music na vyanzo vya habari vya MTO vinasema kuwa Pretty Vee amekuwa akitumia muda mwingi katika jumba kubwa la Rozay lililopo huko Atlanta.
Hivi karibuni rapa huyo alihusishwa kutoka kimapenzi na mrembo kutoka Tanzania Hamisa Mobeto, baada ya kuonekana kuwa pamoja wakifurahia maisha huko Dubai.