You are currently viewing RICK ROSS KUACHIA ALBUM MPYA MWEZI DISEMBA,2021

RICK ROSS KUACHIA ALBUM MPYA MWEZI DISEMBA,2021

Mkali wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani Rick Ross ametangaza tarehe rasmi ambayo album yake mpya itaingia sokoni.

Kupitia ukurasa wake Instagram rozay amesema album yake mpya “Richer Than I Ever Been” itatoka rasmi Disemba 10 mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu jina la album hiyo ya “Richer Than I’ve Ever Been”, Rick Ross amesema kuwa wazo la kuita Album yake hivyo ni kutokana na mazungumzo aliyofanya siku moja na mzee mmoja ambapo alisema, “kiimani mimi ni tajiri na nina utajiri kuliko nilivyokuwa.”

Hii itakuwa ni album ya 11 kwa mtu mzima Rick Ross baada ya ‘Port of Miami 2’ iliyotoka agosti mwaka wa 2019.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke