Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Barbados Mia Mottley kumtaja mwanamuziki Rihanna kama shujaa wa Taifa wa Barbados, ripoti zimemtaja mwimbaji huyo ambae pia ni billionea wa kike, kuwa mjamzito.
Taarifa hiyo inaripotiwa na kuthibitishwa na verified-Twitter account ya The Academy, ikimtaja kuwa na ujauzito wa mpenzi wake rapper Rakim Athelaston Mayers maarufu kama AsAP Rocky
Rocky na Rihanna wamekuwa marafiki wa karibu katika kipindi cha muda mrefu kabla ya kuthibitisha hadharani kuwa wanapendana mwaka wa 2021.
Mwaka wa 2013, Rihanna alitokea katika video ya Asap Rocky ya “Fashion Killa” kama video vixen,jambo ambalo lilihusisha uwepo wa mahusiano ya kimapenzi kati yao