Staa wa muziki kutoka marekani Rihanna amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ujauzito wake kwenye event yake ya Fenty Beauty Universe iliyofanyika Los Angeles Februari 11 mwaka huu.
Akizungumza na Jarida la PEOPLE, Rihanna amefunguka kuhusu changamoto za kuwa mwanamitindo wakati akiwa mjamzito kwa kusema kuwa anafurahia kila hatua ya uja uzito wake na ndio maana anaacha tumbo lake wazi.
Januari 31 mwaka huu Rihanna na AsAP Rocky walitangaza rasmi kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja kwa kuachia picha wakiwa matembezini mjini New York zilizomuonesha Riri akiwa mjamzito.