You are currently viewing RIHANNA ATUNUKIWA CHEO CHA HESHIMA,AITWA SHUJAA WA TAIFA LA BARBADOS

RIHANNA ATUNUKIWA CHEO CHA HESHIMA,AITWA SHUJAA WA TAIFA LA BARBADOS

Sasa unatakiwa kutanguliza neno ‘Mheshimiwa’ pale unapolitaja jina la Rihanna, Novemba 30 mwaka huu msanii huyo ametunukiwa cheo cha heshima kwa kutangazwa kuwa Shujaa wa taifa la Barbados.

Rihanna ametunukiwa wadhifa huo na Waziri Mkuu wa taifa hilo Mia Mottley mbele ya Rais mpya wa nchi hiyo Bi. Sandra Mason kwenye hafla  ya taifa la Barbados kuondoka rasmi kwenye utawala wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza ambao ulidumu kwa miaka 55.

Rihanna  anakuwa shujaa wa 11 katika taifa la Barbados na wa kwanza kutunukiwa tangu mwaka wa 1998.

Riri ambaye amekuwa akipaza sauti kuhusu Barbados na vivutio vyake pia ni balozi wa Utalii katika taifa hilo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke