Staa wa muziki kutoka Marekani , Rihanna kwa sasa amechoshwa na maswali ya mashabiki ya ni lini ataachia Album yake mpya.
Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kjamii ameonekana akirekodi bango lililoandikwa “Drop The Album Rihanna” lililokuwa kwenye kumbi moja ya starehe. Hatua hiyo imewaaminisha mashabiki kuwa rihanna yupo mbioni kukata kiu yao na album mpya hivi karibuni.
Itakumbukwa, mwaka wa 2020 Rihanna kupitia mahojiano na Jarida la British Vogue hivi alieleza kuwa hawezi kusema ni lini Album yake itatoka lakini anafanya kazi kubwa ya kurekodi muziki.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 33, mara ya mwisho kuachia albamu ilikuwa mwaka wa 2016, lakini kulikuwa na taarifa kwamba mwaka wa 2021 ataachia albamu mpya kutokana na uhitaji wa mashabiki zake.