Mwanamuziki Rihanna ameripotiwa kuwa anatengeneza Documentary kuhusu maisha yake kuelekea kwenye tukio kubwa la Super Bowl Halftime show ambayo atatumbuiza mwakani.
Riri amesaini dili la mabilioni ya pesa na kampuni ya Apple, na vipande vya ‘Behind the Scenes’ vya Documentary hiyo vitarushwa.
“Kuna hamu kubwa ya kufanya kila kitu na Rihanna, hasa kipindi hiki ambacho anarejea Jukwaani kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.” chanzo kimoja kilieleza. Camera zitazunguka kuangazia maisha yake kama Mama mpya ambaye alijifungua mtoto mwezi Mei, akijitayarisha kwa ujio mpya kwenye muziki.
“Atakuwa akirekodiwa wakati wa mazoezi (rehearsals) na vikao kuelekea usiku mkubwa wa onesho lake kwenye Halftime show ya Super Bowl. Hii ni kuonesha kwa undani maisha yake yalivyo.” chanzo kilieleza.