You are currently viewing Rihanna na Tems watajwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo ya Oscar

Rihanna na Tems watajwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo ya Oscar

Mwimbaji Temilade Openiyi a.k.a Tems kutoka Nigeria, ameweka Historia ya kuwa Msanii mwenye muda mfupi kwenye Muziki na kufanikiwa kutajwa kuwania Tuzo ya Oscar kupitia wimbo wa LiftMeUp alioshiriki kuuandika pamoja na Rihanna

Licha ya Ukubwa wake kwenye tasnia ya Muziki, kwa mara ya kwanza Mwimbaji Rihanna naye amefanikiwa kuingia kwenye kipengele cha ‘Best Original Song’ kupitia wimbo wa Lift Me Up uliotumika kama Soundtrack ya Filamu ya Black Panther: WakandaForever

Tems amefanikiwa kushinda Tuzo zaidi 30 na ametajwa kuwania zaidi ya Tuzo 80 hadi sasa. Rihanna amekuwa kwenye Muziki kwa takribani Miaka 18 na hadi sasa ana Tuzo 235 na kutajwa kuwania zaidi ya Tuzo 630.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Machi 12, mwaka 2023 huko Jijini Los Angeles nchini Marekani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke