You are currently viewing Ringtone afunguka sababu za kuwaponda Willy Paul na Bahati

Ringtone afunguka sababu za kuwaponda Willy Paul na Bahati

Hitmaker wa Ombi Langu, Ringtone Apoko amefunguka sababu ya kuwakosoa wasanii Willy Paul na Bahati kila mara kwenye majukwaa mbali mbali.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema wawili hao walimvunjia heshima mwenyezi Mungu kwa kutumia vibaya kiwanda cha muziki wa injili kwa ajili ya kujilimbikizia mali na kisha wakageukia muziki wa kidunia.

Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kitendo cha Willy Paul na Bahati kutumia njia haramu kuchuma mali wanayomiliki kwa sasa imewaponza kisanaa kiasi cha kutopata mafanikio kwenye muziki wao.

Katika hatua nyingine Ringtone ametetea utajiri wake kwa kusema kuwa ana vyanzo vingi halali vinavyomuinguzia kipato huku akikanusha tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya ulanguzi wa pesa kwani inakwenda kinyume na maandiko matakatifu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke