Msanii wa nyimbo za Injili nchini Ringtone Apoko ni kama amekataa tamaa kwenye mchakato wa kutafuta mke wa ndoto yake.
Hii ni baada ya hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” kukiri hadharani kwamba hana msukumo tena wa kumtafuta mke.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Ringtone amesema kwa sasa amehamua kuelekeza nguvu zake kwenye ishu ya kueneza injili wakati anasubiri Mungu ajibu maombi yake.
Ikumbukwe mwaka wa 2019 Ringtone aliwaacha mashabiki zake na maswali mengi baada ya kuonekana na bango ambalo lilikuwa limeanisha sifa zote ambazo anazitafuta kwa mwanamke wa ndoto yake.
Wengi walidhani ni kiki lakini Ringtone mwenyewe alikuja akakanusha madai hayo kwa kusema kwamba alikuwa serious kwenye suala la kumtafuta mke.