Msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone amemtolea uvivu mwanahabari mwenye utata nchini Andrew Kibe kwa madai ya kuikosoa ndoa ya msanii Guardian Angel na mke wa Esther Musila.
Kupitia instagram page yake Ringtone amemtaka kibe aheshimu maamuzi ya Guardian Angel na mke wake Esther Musila kuhalilisha ndoa kwa njia ya harusi ikizingatiwa kuwa ni watu wazima ambao upendo uliwaleta pamoja licha ya utofauti wa umri wao.
Hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” ameenda mbali na kumshauri Kibe akome kuingilia maisha ya wana ndoa hao wawili na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye shughuli itakayomuingizia kipato kwani anapoteza muda wake kuzungumzia jambo ambalo litamsaidia maishani.
Kauli ya Ringtone imekuja mara baada ya Andrew Kibe kuonekana kukejeli ndoa ya Guardian Angel na mke wake Esther Musila kwa kusema kwamba haoni ndoa hiyo ikidumu kwani msanii huyo aliwavunjia heshima vijana wa Kenya kwa hatua kumuoa mwanamke mkubwa kiumri.