You are currently viewing RINGTONE AMKASHIFU NYANSHINSKI KUTOKANA NA TAMASHA LAKE LA SHIN CITY

RINGTONE AMKASHIFU NYANSHINSKI KUTOKANA NA TAMASHA LAKE LA SHIN CITY

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Ringtone amemtolea uvivu rapa Nyashinski baada ya kuandaa tamasha lake la Shin City wikiendi hii iliyomalizika.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ringtone amesema kwamba inasikitisha kuona msanii wa haiba ya Nyashinski anaendekeza ufuska na uesharati wakati yeye kama msanii wa injili anaendeleza harakati za kubadilisha kizazi kijacho.

“WE IS INVESTING AT FUTURE GENERATIONS AND NYASH @realshinski IS BUSY HELPING PEOPLE DO FONICATE AND ADULTERY SHAME AT U FOR DEMON POSSESSION CONCERT AT CARNIVORE “, Aliandika Ringtone.

Kauli hiyo ringtone imeonekana kuwakasirisha watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wamemtaka aache kuwaonea wasanii wengine wivu kwa mafanikio yao na badala yake aandae tamasha lake la muziki litakalo muingizia kipato.

Utakumbuka Aprili 16 mwaka Nyashinski alijaza nyomi la mashabiki katika ukumbi wa Carnivore huko Jijini Nairobi ambako walipiga show ya kufa mtu iliyowaacha mashabiki wakiwa na kiu ya kutaka burudani Zaidi kuptia tamasha lake la Shin City.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke