Msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone amemchana msanii mwenzake Size 8 kwa kitendo cha kujaribu kumtoa mapepo muumimi moja wiki moja iliyopita.
Katika mahojiano yake na Presenter Ali, Ringtone amesema Size 8 hana uwezo kuwaomba wakristo hadi kuwatoa mapepo huku akisema kwamba msanii huyo anatumia njia hiyo kujitafutia umaarufu.
Kauli hiyo imekuja wiki moja baada ya video ya Size 8 akimuombea muumini moja kanisani kusambaa mtandaoni jambo ambalo lilizua mjadala mzito miongoni mwa wa kenya wengi wakidai kuwa msanii huyo ana uwezo wa kumtoa mtu mapepo.