Imekuwa kawaida sasa kwa mastaa Duniani kumwaga mamilioni ya pesa hasa kwenye vito vya thamani, magari pamoja na majumba ya kifahari
Msanii wa nyimbo za Injili nchini Ringtone ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho.
Mkali huyo wa “Sisi ndio tuko” ametumia kiasi cha zaidi ya shillingi milioni 60 za Kenya kununua saa mpya aina ya Richard Mille Watch.
Hii ni Kwa mujibu wa risiti ya ununuzi wa saa hiyo ambayo aliishare kwenye insta story yake kwenye mtandao wa Instagram.
Ringtone anaungana na mastaa kama Davido, Drake, Jay Z, Kanye West ambao hupendelea kuvaa saa za aina ya Richard Mille Watch