Mwànamziki wa nyimbo za injili nchini Ringtone Apoko amepewa makataa ya siku kumi kuondoka kwenye nyumba anayoishi mitaa ya Runda jijini Nairobi.
Kulingana na barua ya kampuni ya mawakili ya AGN Kamau Advocates, nyumba ambayo ringtone anaishi ni ya raia wa Sweden kwa jina Mona Ingegard aliyefariki mwaka wa 2007 na Ringtone alinunua nyumba hiyo bila kufuata njia sahihi.
Hata hivyo Ringtone ambaye amekuwa akijinadi kwamba ni mwanamuziki utajiri afrika mashariki hajatoa tamko lolote kuhusiana madai yaliyoibuliwa na kampuni ya wanasheria ya AGN Kamau Advocates.