You are currently viewing RINGTONE APINGA AZMA YA WILLY PAUL KUJITOSA KWENYE ULINGO WA SIASA MWAKA 2022

RINGTONE APINGA AZMA YA WILLY PAUL KUJITOSA KWENYE ULINGO WA SIASA MWAKA 2022

Baada ya Willy Paul kutangaza azma ya kujiunga na siasa mwaka wa 2022, msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone ameonekana kutofautiana kimawazo na Hitmaker huyo wa “Lenga”.

Akipiga stori na Mungai Eve kwenye mtandao wa Youtube Ringtone amesema watu wasichukulie kauli ya Willy Paul kwa uzito kwani msanii huyo anajaribu kushinda na msanii mwenzake Bahati ambaye kipindi cha nyuma alitia nia ya kuwania ubunge wa Mathare.

Hitmaker huyo wa “Pamela” amemshauri Willy Paul aachane na siasa na badala yake awekeze nguvu zake kwenye muziki kwani ni mmoja wa wasanii ambao wana kipaji cha kipekee nchini.

Sanjari na hilo Ringtone amedokeza kwamba mwaka wa 2022 ataweka wazi azma yake ya kujiunga na siasa kwani amekuwa akipata shinikizo za kuwania ubunge Dagorreti kaskazini kutoka kwa watu wake wa karibu.

Ikumbukwe mwaka wa 2011 Ringtine aliwania ubunge katika uchaguzi mdogo wa Kitutu Masaba kupitia chama cha Vijana Progressive Party ambapo aliibuka wanane kwa kupata kura 467.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke