Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone ameamua kutaja kiasi cha pesa anacholipisha kwa show zake iwapo utahitaji kufanya kazi nae.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Ringtonr ametangaza kuwa analipisha kwa show moja shillingi millioni 1 na shilling million 1.5 za Kenya kutokea kwenye klabu (Club Appearance).
Ringtone ambaye juzi kati alitangaza kujiunga na muziki wa kidunia amesema amechukua hatua hiyo kutokana na mapromota kumhitaji sana kwenye shughuli zao kwani amekuwa akitoa muziki mzuri.
Lakini pia ametangaza kubadilisha jina lake la usanii kutoka kwa Ringtone kwenda kwa Blingtone huku akiri kuwa mapato ya nyimbo zake za Injili ambazo aliziimba kipindi cha nyuma itaenda kwa watoto mayatima.
Ringtone amedokeza ujio wa ngoma yake mpya ambayo itaingia sokoni wiki hii ikiwa ni siku chache zimepita tangu atangaze kuanza kuimba nyimbo za mapenzi.