You are currently viewing RINGTONE APOKO ATANGAZA KUACHA MUZIKI WA INJILI

RINGTONE APOKO ATANGAZA KUACHA MUZIKI WA INJILI

Nyota wa muziki kutoka Kenya Ringtone amezua mjadala mkali kwenye  mitandao ya kijamii mara baada ya kutangaza kuachana na kazi za sanaa ya muziki wa injili.

Kupitia video aliyoichapisha kupitia ukurasa wake wa Instagram ringtone ameweka wazi kwamba ameamua kujiunga rasmi na muziki wa kidunia ambapo sasa atajikita kwenye uimbaji wa nyimbo za mapenzi.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Pamela amewashukuru mashabiki zake waliofuatilia nyimbo zake kipindi alikuwa anajihusisha na uimbaji wa nyimbo za injili huku akitoa wito kwa wakenya kumuunga mkono kwenye safari yake mpya ya muziki wa kidunia.

Hata hivyo amewataka wasanii wanaofanya muziki wa kidunia wampe ushirikiano kwa kuwa hajajiunga na muziki huo kwa ajili ya ushindani bali kuupeleka muziki wa kenya kimataifa.

Ni jambo ambalo limewachanganya mashabiki zake japo kufikia sasa hajataja hasa chanzo cha kufikia uamzi huo ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahoji kuwa huenda mwanamuziki huyo alikuwa akipitia changamoto flani kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini Kenya.

Ikumbukwe kwamba huyu sio msanii wa Kwanza kutoka Kenya kusitisha safari yake ya muziki wa injili na kujiunga na muziki wa kidunia, tumewaona pia wasanii kama Willy Paul, Bahati, Mr. Seed, Weezdom ambao kipindi cha nyuma walikuwa waimbaji wa nyimbo za Injili wakigeukia muziki wa kidunia.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke