You are currently viewing RINGTONE APOTEZA MILLIONI 3 ZA KENYA BAADA YA WIMBO WA YESU ANG’ARE KUFUTWA YOUTUBE

RINGTONE APOTEZA MILLIONI 3 ZA KENYA BAADA YA WIMBO WA YESU ANG’ARE KUFUTWA YOUTUBE

Msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone ameumizwa na kitendo cha wimbo wake uitwao Yesu Ang’are aliyomshirikisha Rose Muhando kufutwa kwenye mtandao wa youtube kwa madai ya haki miliki.
 
Kupitia ukurasa wake wa instagram Ringtone amesema  anakadiria hasara ya shillingi millioni tatu alizotumia kutayarisha audio na video ya wimbo huo jambo ambalo amesema limempelekea kupata na msongo wa mawazo.
 
Ikumbukwe wimbo wa yesu Ang’are kutoka kwa mtu mzima Ringtone ulifutwa kwenye mtandao wa youtube baada ya ringtone kushindwa kumaliza tofauti zake na lucy ndanu aliyewasilisha lalama kwenye mtandao wa youtube kuwa rose muhando alitumia mashairi ya wimbo wake kwenye wimbo wa ringtone.
 
 
 
 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke