Miongoni mwa mijadala mikubwa kwenye kiwanda cha burudani nchini ni saa ya bei ghali aliyonunua Ringtone aina ya Richard Millie mwishoni mwaka wa 2021 aliyodai kuwa ameinunua kwa shilingi milioni 47 za Kenya na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee nchini anayemiliki saa hiyo.
Taarifa ikufikie kwamba, ishu hiyo imezua tafrani ya aina yake kwenye mitandao ya kijamii baada ya Kurasa moja mtandaoni maarufu kama Fake Watch Busta kuchapisha taarifa kuwa msanii huyo alikuwa amevaa saa feki.
Kulingana na Fake Watch Busta saa ya Ringtone imekosa baadhi ya nakshi zinazopatikana kwenye saa Original ya Richard Millie.
Hata hivyo suala hilo limeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa walikuwa wanafahamu saa hiyo ni batili ikizingatiwa kuwa Ringtone amekuwa akiishi maisha ya kuigiza.