You are currently viewing RINGTONE ATAMBA NA SURUALI YA SHILLINGI MILLIONI 1.5 ZA KENYA

RINGTONE ATAMBA NA SURUALI YA SHILLINGI MILLIONI 1.5 ZA KENYA

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Ringtone ameingia kwenye headlines kwa mara nyingine, mkali huyo kwa sasa amekuwa ni mtu wa kutupa Breaking News kila uchao hii ni baada ya kusema kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza Kenya kumiliki suruali ghali zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone ameeleza kuwa licha ya kuwa ana miliki suruali yenye thamana ya shilllingi millioni 1.5 Za Kenya hajawahi kuwa na jeuri ya kutaka kujionesha kuwa ana pesa nyingi kama namna vijana wa siku hizi wanavyofanya mtandaoni.

Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa Ringtone kutamba kuhusu kumiliki vitu vya thamani kwani mwaka wa 2021 alitusanua kuwa alinunua saa ya shillingi milioni  60 za Kenya aina ya Richard Mille Watch.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke