You are currently viewing RINGTONE ATIA NENO SAKATA LA WILLY PAUL NA DIANA MARUA

RINGTONE ATIA NENO SAKATA LA WILLY PAUL NA DIANA MARUA

Baada ya sakata la Willy Paul na Diana Marua kugonga vichwa vya habari nchini Staa wa muziki wa injili Ringtone ameamua kuvunja kimya chake juu ya suala hilo.

Akipiga stori na online Media Ringtone ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba Wakenya wamechoshwa na kile ambacho kinaendelea kati ya Willy Paul, Bahati na Diana Marua, hivyo pana haja ya watatu hao kuzika tofauti zao na waelekeze nguvu zao kwenye ishu ya kuupeleka muziki wao kimataifa.

Hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” amewaomba wadau wa muziki nchini kuingilia kati sakata la Willy Paul na Diana Marua ambalo linaendelea huko mtandaoni kwani wasanii hao wakiachwa jambo baya litakuja kutokea.

Ikumbukwe Willy Paul na Diana Marua wamekuwa wakirushiana maneno makali mitandaoni mara baada ya Diana Marua kuibua tuhuma za kubakwa na bosi huyo wa Saldido miaka kadhaa iliyopita

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke