You are currently viewing RINGTONE ATOA OFA YA KUWASAIDIA WAJANE KENYA

RINGTONE ATOA OFA YA KUWASAIDIA WAJANE KENYA

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Ringtone ametangaza kutoa ofa ya kumlipia karo mwaka ya mmoja watoto wa akina mama wajane waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kitaifa wa darasa la nane uliokamilika majuzi.

Ringtone amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram ambapo amesema atatoa usaidizi huo kwa mtoto wa mama mjane ambaye alipata alama zaidi ya 400 kwenye mtihani wake wa K.C.P.E

Hitmaker huyo wa ngoma ya Zoea mawe amedai atatoa ofa hiyo kwa mjane yeyote ambaye atamtumia ujumbe wa kwanza kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram huku akiwahimiza wasanii wenzake kushindani kwenye masuala ya kurudisha fadhila kwa jamii.

“ Nataka kuongea na single mothers, kama uko na mtoto alifanya class 8 na akapata marks over 400, unidm nataka kukusaidia kulipa school fees ya mtoto wako kwa mwaka mmoja. Single mothers wenye mtoto wake alipata maraks over 400 kwa KCPE…nataka kukusaidia . Ule ataniDM wa kwanza ndio ntarushia school fees ya 1 year… ntarrepost hapa hapa na mtsaema naringa …tucompete kufanya mazuri” Ameandika Ringtone.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kupuzilia mbali madai hayo ya Ringtone kwa kusema kwamba msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumzia nchini ikizingatiwa kuwa amezoea kutumikia kiki kwenye muziki wake

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke