Balaa linazidi kumuandama staa wa muziki nchini Ringtone, baada ya babay mama wake kujitokeza na kudai kuwa msanii huyo amewatelekeza watoto wake.
Mwanamke huyo ambaye anadai ana watoto wawili na Ringtone, amesema msani huyo amegoma kabisa kutotoa pesa za huduma ya matumizi kwa watoto wake licha kumshinikiza kufanya hivyo mara kwa mara
Aidha mwanamke huyo amedai kuwa kwa sasa anapitia wakati mgumu wa kumlea mtoto huyo kwa sababu hana kazi na hapati msaada wowote kutoka kwa Ringtone ambaye anaingiza pesa nyingi kupitia muziki wake.
Hata hivyo Ringtone hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai yaliyoibuliwa na baby mama wake huyo kuwa amemtelekeza watoto wake.