You are currently viewing RINGTONE AWEKA WAZI SABABU ZA KUUKIMBIA MUZIKI WA INJILI

RINGTONE AWEKA WAZI SABABU ZA KUUKIMBIA MUZIKI WA INJILI

Msanii asiyeishiwa na vituko kila leo kutoka nchini Kenya Ringtone Apoko kwa mara ya kwanza ameamua kuweka wazi sababu za kuacha muziki wa injili.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Ringtone amesema wanawake ndio walimpelekea kuchukua maamuziki magumu ya kuacha muziki wa injili na kugeukia muziki wa kidunia.

Hitmaker huyo wa Sisi ndio Tuko ameenda mbali zaidi na kusema kwamba wanawake wengi nchini wamesusia kufuata Yesu Kristo na badala yake wameanza kumpenda kimapenzi jambo ambalo limemkatisha tamaa kwenye harakati zake za kusambaza injili kupitia nyimbo zake.

Hata hivyo amesema ameamua kuchukua mapumziko mafupi kwenye muziki wake ili wanawake wanaomtaka kimapenzi wamwaache na kumrudia Yesu Kristo mwana wa Mungu.

Kauli hiyo Ringtone imeibua maswali mengi miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa msanii huyo anatumia suala la kuacha muziki wa injili kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mitandaoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke