You are currently viewing RINGTONE AZUA GUMZO MTANDAONI,AACHIA ORODHAA YA MASTAA 10 TAJIRI NCHINI KENYA

RINGTONE AZUA GUMZO MTANDAONI,AACHIA ORODHAA YA MASTAA 10 TAJIRI NCHINI KENYA

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko ameingia kwenye headlines mara baada ya kujitengenezea orodha ya mastaa tajiri nchini Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone amejiweka kwenye nafasi ya kwanza huku akidai kuwa ana nyumba tano za kifahari katika mitaa ya Runda, Karen na muthaiga huku akieleza anamiliki hoteli na nyumba kadhaa za makazi, magari 7 aina ya Range Rover, Maybach, na BMW.

Nafasi ya pili kwenye orodha hiyo ni, amemtaja mbunge wa eneo la Starehe Kaunti ya Nairobi, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar, ambaye kwa mujibu wake anamiliki nyumba mbili na magari matatu.

Kwenye orodha hiyo pia amewataja wasanii kama Akothee ambaye ana Jumba moja la kifahari,na gari aina SUV, pamoja na Bahati ambaye ana magari 3 na majumba 3 ya kifahari.

Mastaa wengine ambaye wametajwa ni pamoja na Khaligraph Jones, Arnelisa Muiga, Krg The Don, Betty Kyalo, Huddah Monroe, Otile Brown, na mwisho kabisa Size 8 pamoja na mume wake DJ Mo huku akisisitiza kuwa ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo.

Hata hivyo mkali huyo wa ngoma ya “Sisi ndio tuko” ameahidi kutoa orodha nyingine ya watu maarufu nchini Kenya ambao amesema ni wapiga kelele ilhali hawamiliki chochote.

Orodha ya Ringtone imeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake kwenye mitandao ya Kijamii ambao wameenda mbali zaidi kumtolea uvivu msanii huyo wakidai kwamba kama kweli angekuwa tajiri angeonekana kwenye orodha ya wasanii tajiri iliyotolewa na jarida la Forbes mwaka wa 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke