You are currently viewing RINGTONE: HUDDAH MONROE ALINITAKA KIMAPENZI NIKAMKATAA

RINGTONE: HUDDAH MONROE ALINITAKA KIMAPENZI NIKAMKATAA

Mwanamuziki wa nyimbo za Injil nchini, Ringtone Apoko amedia kuwa mrembo maarufu mtandaoni nchini, Huddah Monroe aliwahi kumtongoza lakini akamkataa.

Kauli yake inakuja mara baada ya Huddah kuibuka na kudai kuwa hajaona mwanaume ambaye amekidhi vigezo vya kuwa naye nchini Kenya.

Sasa  Ringtone ameibuka na kusema “Tumekuwa na safari refu sana ya maisha na Huddah Monroe, tunajuana sana kwa vilemba, hawezi sema hivyo, umejuana miaka mingi. Ametoka mbali, labda alikuwa anatafuta kiki ama alikuwa amelewa, huwa anakunywa sana msimhukumu.

Ameendelea kwa kusema,  “Hawezi sema mimi sio mtanashati na alikuwa ananililia kitambo, mimi ndio nilimkataa, alikuwa ananililia na kunisumbua sana eti ananitaka nikamkataa”

“Alinitongoza nikakataa, nilimwambia lazima aokoke ndivyo tuweze tuzungumzia mambo mengine. Ni msupu. Yeye ni mmoja wa wanawake warembo zaidi barani Afrika. Hata hivyo hawezani nami kwa kuwa lazima aokoke, atubu dhambi na amkiri Yesu. Hapo ndipo tulikosania. Nilimkataa kabisa”. amesema Apoko.

Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameonekana kumshangaa sana Ringtone kwa kauli yake hiyo ambayo wamedai hakuna namna ambavyo Huddah Monroe anaweza kumtaka kimapenzi ikizingatiwa kuwa hana vigezo kabisa vya kumshawishi mrembo atokee nae kimapenzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke