You are currently viewing RIPOTI YA UCHUNGUZI ILIYOFANYWA NYUMBANI KWA ASAP ROCKY IMETOKA

RIPOTI YA UCHUNGUZI ILIYOFANYWA NYUMBANI KWA ASAP ROCKY IMETOKA

Ripoti ya uchunguzi uliofanywa nyumbani kwa rappa A$ap Rocky, hatimaye imetoka, ambapo inadaiwa polisi wamekuta bunduki kadhaa na kitu pekee ambacho hakikuwekwa wazi ni kama Je, polisi waliipata Bunduki halisi iliyotumika kumpiga mtu risasi wakati wa mabishano kwenye tukio lilitokea huko Hollywood au la.

Kwa mujibu wa TMZ, vyanzo vya utekelezaji wa sheria (Law enforcement sources) vinasema wapelelezi watafanya majaribio ya silaha moja baada ya nyingine ili kubaini ikiwa Rocky ndiye mhusika mkuu wa shambulio hilo, pia imedokezwa kuwa polisi watafuatilia historia ya bunduki ili kubaini zilikotoka, nani alizinunua au kama zimeripotiwa kuibwa sehemu yeyote.

Taarifa ya awali ilieleza undani wa namna Rocky alivyokamatwa katika uwanja wa ndege LAX alipokuwa ameshuka katika ndege binafsi wiki iliyopita wakati yeye na Rihanna wanarudi kutoka mapumzikoni huko Barbados.

Ikumbukwe, Rocky alifunguliwa kesi hiyo kufuatiwa kuhusishwa na tukio la kushambulia kwa kutumia silaha, kwa madai ya kuwa aliwafyatulia risasi watu kadhaa na kusababisha taharuki huku mtu mmoja akiripotiwa kujeruhiwa katika sehemu ya mkono wake mwezi Novemba 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke