Mwanablogu aliyegeukia siasa nchini Robert Alai amekosoa pendekezo la Nameless kutaka barabara moja jijini Nairobi lipewa jina la marehemu E-sir kama njia moja ya kutambua mchango wake katika tasnia ya muziki nchini.
Kulingana na Alai pendekezo la Nameless limepitwa na wakati na ingekuwa vyema kituo cha kukuza vipaji vya wasanii ingebuniwa na kisha kupewa jina la msanii huyo aliyeachana alama kwenye muziki wa kizazi kipya.
Utakumbuka Gavana Nairobi Johnstone Sakaja tayari aliunga mkono pendekezo hilo ila akataka taratibu za kisheria kufuata kabla ya ombi hilo kufanikishwa.
Nameless anaendeleza harakati za kurai wakenya kutia saini mswaada wa kushinikiza barabara moja jijini Nairobi maeneo ya South C kupewa jina la msanii E-Sir kabla hajaidhinishwa.