You are currently viewing RODDY RICCH KUWAFARIJI WAHANGA WA TAMASHA LA TRAVIS SCOTT

RODDY RICCH KUWAFARIJI WAHANGA WA TAMASHA LA TRAVIS SCOTT

Rapa kutoka nchini Marekani Roddy Ricch alikuwa kwenye orodha ya wasanii ambao wangetumbuiza kwenye siku ya pili ya tamasha la Astroworld Music Festival mjini Houston, sasa ametangaza kutoa pesa zake ambazo alilipwa na kwamba zitakwenda kuwafariji wafiwa na wahanga wa tukio lililotokea kwenye onesho la kwanza, Novemba 5.

Tamasha hilo ambalo liliandaliwa na Travis Scott kwa lengo kusaidia elimu kwa vijana wadogo, lilikumbwa na simanzi mara baada ya watu takribani 11 kufariki dunia na wengine kujeruhiwa wakati onesho hilo likiendelea, hivyo kupelekea kuahirishwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke