Jarida maarufu na kongwe nchini Marekani Rolling Stone limeutaja wimbo wa Wizkid ‘ESSENCE’ aliyomshirikisha Tems kama wimbo bora wa mwaka 2021 huku ukikamata namba 1 kwenye orodha ya ngoma 50 za wasanii kutoka kila pembe ya dunia.
Orodha hiyo hutolewa kila mwaka ikijimuisha ngoma 50 bora duniani zilizofanya vizuri kwa mwaka husika. Ngoma za wasanii wenye majina makubwa kama Taylor Swift, Olivia Rodrigo, BTS, Bruno Mars, Billie Ellish, Adele zimekalishwa na mbabe huyo kutoka nchini Nigeria.