Msanii kutoka nchini Uganda Ronald Alimpa ameripotiwa kukamatwa kufuatia hatua ya kususia show zake tatu ambazo alipaswa kutumbuizwa Disemba 25 na 26 mtawalia.
Kushindwa kwake kutumbuiza kwenye show hiyo kuliwafanya mashabiki wenye ghadhabu waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, kuharibu mali ya mamillioni ya fedha iliyowaacha mapromota wakikadiria hasara kubwa.
Hitmaker huyo wa “Seen Don” ambaye amekuwa akiuguza majeraha ya ajali aliyoipata miezi kadhaa iliyopita,alipaswa kutumbuiza kwenye show hiyo akiwa kwenye kiti cha magurudumu kutokana na kupoteza miguu yake katika ajali hiyo.
Kwa sasa tunasubiri tamko la meneja wa Ronald Alimpa kunyoosha maelezo juu ya msala wa kukamatwa kwake lakini pia chanzo cha kutofika kwenye eneo la show kwa wakati licha ya kulipwa pesa zote.